Mtazamo wa chuo kuhusiana na korona

Janga la korona limekua likileta taharuki na wasiwasi mkubwa miongoni mwa jamii, ikiwemo Chuo cha sayansi ya Afya Kolandoto.
Kwa kujua umuhimu wa kujikinga na marathi hayo chuo chetu kimechukua hatua madhubuti ili kuhakikisha kwamba wanafunzi na wafanyakazi wote wanakua salama, Hilo linahusisha kuvaa barakoa, kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu na kuweka vitakasa mikono katika sehemu nyingi za chuo


Angalizo: Kumbuka Kunawa Mikono Kwa maji Safi Yanayotiririka na Sabuni Mara Kwa Mara. Kaa nyumbani na upunguze safari zisizo za lazima! Pasipo na maji tumia kitakasa mikono (Sanitizer) na uvae Barakoa (Mask) muda wote. Corona ipo na inazuilika tukizingatia maelekezo toka Wizara ya Afya na mamlaka zinazohusika.